Rapcha - Interview (Official Music Video)

  • To The Top Vol.1 (Special Edition)
    Stream & Download: bit.ly/3xRmbjb
    TRACK #2 INTERVIEW
    LYRICS:
    Asubuhi flani ya hang over bwii
    Nani tena huyu ananipigia saa hii
    Napapasa kuitafuta simu mpaka naikamata,
    macho kwenye screen naona jina “GACHI B”
    We mshezi una balaa hatari
    Sjui zilikua ni tungi au vijiti walimix wale
    Uliwaka ukavamia dem wa mtu ukamshika shika
    Na ukawa unaforce kumkiss eti palepale
    Nlijua lazma utani-roast
    Sjawahi waka vile mpaka ikatokea hadi data zime-lost
    Mchizi alinitwika ngumi bufff kwenye mdomo yani nkahisi nmepoteza meno yote on the spot
    Usingeweza kutoboa pale
    Ilibidi ncheki gap tuchomoke tukimbie mbali
    Nlikudrop kwako ukanambia nkushtue mapema
    Una interview ya kazi leo katafte ugali
    Ayaaa nahisi nshachelewa
    Duhh mchongo bado nusu saa nkichelewa hawatonielewa
    Umetisha kunishtua acha niwahi chap nkawaskie nikitoka ntadondoka studio
    oyeah
    Haya
    Mswaki dakika moja, kuoga dakika moja
    Suruali ya kitambaa imejikunja na iko moja
    Ila haya yote ningeandaa tangu jana isingekua kazi fresh nitanyoosha daika moja
    Naboost simu isinizimikie nkiwa njiani
    Muda unaenda sana sa inabidi ntoke ndani
    Navaa chap uber njoo nifate sinza vatcani
    Sina muda wakuelekeza fata ramani
    Dakika mbili uber akafika
    Madevera smart kama wewe mjini ndo wanahitajika
    Skia Nirushe chap posta pale 99 plaza ntakuongeza buku 5 tukiwahi kufika
    Palepale kwanza dreva kawaka
    Daah leo ka bahati yani mzee wa lissa nimekunyaka
    Hivi kwenye ule wimbo ulipigwa kweli?
    Sioni hata makovu na ile story vipi ishakukuta kweli!??
    Sasa hapa ndo tutapochelewa
    Focus yako iwe kwenye kuniwahisha na sio kuongea
    Mgenilipa kama mnavyonisifia
    Saivi nsingekua busy kutafuta kazi nisiyoielewa
    Hii ndo shida ya wasanii bongo
    Mbele ya camera wapole sana na kujisifia uongo
    Mnasema mnatupenda mashabiki
    Ila tunapokutana mnatutreat kama vile tunanuka shombo
    Na ndo shida ya mashabiki wa bongo
    Mnapenda tu kupuuzia ukweli na kuamini uongo
    Mnasahau ka na si ni binadamu kuna muda tuna stress zetu mtuvumilie kidogo
    Muda unaishia afu bado kuna umbali
    Nikamlipa dreva nikashuka kwenye gari
    Psss psss boda niwahishe posta chap tu
    Zimebaki dakika 5 ufike muda wa interview
    Mbio mbio mpaka destination
    Zimebaki dakika mbili tu afu mchiz ndo naingia reception
    dada wa mapokezi akafurahi aliponiona
    Si akataka alete story nkaona ananichoma
    Nkiwa palepale reception
    Najibizana huyu sista, haki nimechoshwa na questions
    Wakaingia watu wawili ndani
    yule dada alivyowasalimia ikabidi nkae attention
    Nageuka nione kuna nani
    Ndo namuona yule dada ambae jana nilimfata nkamletea uhuni
    Pembeni yake kaongozana na mumewe alieyataka kunitoa meno na ndio boss wa kampuni
    Ilinichukua ka nusu sekunde kukumbuka ule uzito wa ile ngumi kwenye lile tukio
    Nkakamata bahasha ya vyeti vyangu kwa makini nkatazama mlango ulipo vvvuuum nkatimua mbio

    Audio produced & mixed by: instagram.com/gachib/
    Video directed by: instagram.com/majagiking/

    Apple Music: apple.co/3Hs0oBy
    Spotify: spoti.fi/3MXGyiJ

    Join Our Family:
    instagram.com/rapcha_tz/
    twitter.com/rapcha_tz/
    www.tiktok.com/@rapcha_tz

    #rapcha #interview #tothetopvol1specialedition

    Category : Interviews and Podcasts

    #rapcha#interview#official#music#video

    0 Comments and 0 replies
arrow_drop_up